Mashabiki wengi na wapenda soka walibashiri kuwa Washika Mtutu hao
wangewafunga mahasimu wao wa London na kujikita kileleni, lakini bao la
Diego Costa la dakika ya 23 liliwawezesha Blues ambao wamekuwa wakihaha
msimu huu wameifunga timu ya Arsene Wenger mara mbili.
Hapakuwa na msaada wowote pamoja na beki Per Mertesacker kuonyeshwa
kadi nyekundu baada ya kumwangusha Costa dakika tano kabla ya goli
kupatikana, Mjerumani huyo alipokuwa mtu wa mwisho na kumweka straika
huyo wa Chelsea chini. habari zaidi

No comments:
Post a Comment